- INTUITION -
Kabla Sijaendelea Hii Ni Tabia Ya Mwisho Kabisa
Kati Ya Tabia 9 Ambazo Nimeshiweka Hapa
Kama Bado Hujafanikiwa Kuzisoma
Tafafadhali Zisome Na Uanze Kuchukua Hatua
Kwenye Tabia Ambazo Unaona Zinakukwamisha
Ok,,, Tuendelee Kwenye Tabia Ya Mwisho
,,,
Kuna Muda Unakaa Kimya…
Halafu Ghafla Wazo Linakuja Kichwani.
Sio Wazo La Kawaida.
Ni Wazo Ambalo Unalihisi Kabisa Ndani Yako.
Unajua Kabisa:
"Hiki Kitu Natakiwa Kukifanya."
Inaweza Kuwa:
- Kuanza Kitu Fulani
- Kubadilisha Mwelekeo
- Kuacha Kitu Kisichokufaa
Kwa Sekunde Chache Unakuwa Na Uhakika.
Lakini Baada Ya Muda Kidogo…
Akili Inaanza Kuingilia.
- “Je Kama Haitafanya Kazi?”
- “Je Kama Si Sahihi?”
- “Ngoja Niache Kwanza…”
Unaamua Kupuuza.
Unarudi Kwenye Maisha Ya Kawaida.
Na Polepole…
Lile Wazo Linaanza Kupotea
Hii Ni Hali Ambayo Watu
Wengi Wamewahi Kuipitia.
Unapata Hisia Ya Ndani Inayokuongoza.
Lakini Unaipuuzia.
Siku Zinapita.
Halii Hii Ina Uwezo Wa Kujirudia
Mara Kadhaa Na Mara Nyingine
Huwa Kuna Watu Wanakuja
Kwa Namna Ya Ajabu Kukumbusha
Kitu Kile Kile Ambacho Kilikujia Kama Wazo
Na Mara Nyingi Tukio Hili Likitokea Huwa Unajiuliza
"Hiki Kitu Nilihisi Kabisa Ndani Yangu…"
Na Ikishatokea Ghafla Unaanza Kujilaumu
Utaniuliza:
"Francis, Hii Sauti Ya Ndani Ni Nini Hasa?"
Ni Ule Uwezo Wa Ndani Unaokuonyesha Mwelekeo.
Sio Kelele.
Ni Hisia Tulivu Inayokuambia:
“Jaribu Hii.”
Tatizo Ni Hili.
Watu Wengi Wanaizima Kwa:
• Hofu
• Mashaka
• Maoni Ya Watu Wengine
Na Kadri Unavyoizoea Kuipuuzia…
Ndivyo Inavyopungua Nguvu.
Ufanini Basi...
Kama Unataka Kubadilisha Maisha Yako…
Anza Kuisikiliza Sauti Yako Ya Ndani.
Sio Kila Wazo Unapaswa Kulifuata.
Lakini Yale Ambayo:
- Yanajirudia Mara Kwa Mara
- Yanakupa Hisia Ya Ndani
- Yanakuonyesha Mwelekeo
Yape Nafasi.
Anza Na Hatua Ndogo.
Jaribu.
Angalia Yanaenda Wapi.
Kwa Sababu Ukweli Ni Huu:
Mwelekeo Wa Maisha Yako Mara Nyingi Unaanza Na Sauti Ndogo Sana Ndani Yako.
Usipoisikiliza…
Inaweza Kukupita Kimya Kimya.
Na Hapo Ndipo Watu Wengi Huja Kugundua
Kitu Kimoja Wakiwa Wamechelewa Kidogo…
Kwamba Walikuwa Na Majibu Ndani Yao
Tangu Mwanzo… Lakini Hawakuyasikiliza.
...
Nitaziweka Tabia Zote 10 Ndani
Ya PDF Moja Then Nitashare Na Wewe Hapa
Bure Kabisa Ambapo Unaweza Mtumia
Rafiki, Ndugu, Mtoto Wako N.K
Asante Sana...
...
FRANCIS | ABRACADABRA