Kuna Siku Unaamka Na Nguvu Sana.
Unaamua:
"Leo Nafanya Kazi Kweli."
Unaanza Vizuri Bila Shida Yoyote.
- Unafanya Kazi Kwa Bidii.
- Unakuwa Focused.
- Unajisikia Kama Umebadilika Kabisa.
Lakini Siku Inayofuata…
Hali Ni Tofauti.
- Hamasa Haipo.
- Nia Haipo.
- Unajisikia Mzito Tu.
Unaanza Kujiambia:
"Ngoja Nitafute Motivation Kwanza."
- Unatafuta Video.
- Unasikiliza Motivational Speech.
- Unajipa Moyo Kidogo.
Siku Hiyo Unafanya.
Lakini Kesho Yake Tena…
Unarudi Pale Pale.
Na Mzunguko Unaendelea.
Francis Anajua Haya Yote...
Kwanini Kwasababu Amengundua Kuwa
Watu Wengi Wanaishi Hivi Bila Hata Kugundua.
Kwasababu... Wengi Wanategemea
Motisha/Motivation Ili Kuweza Kupiga Kazi Sana
Lakini Siku Motisha Inapopotea…
Kila Kitu Kinasimama.
Ndiyo Maana Kuna:
- Kuanza Kwa Nguvu Sana
- Kisha Kupotea Ghafla
- Halafu Kuanza Tena Baada Ya Muda
Na Maisha Yanabaki Kwenye Mizunguko Ile Ile.
"Repetition Loop"
Utaniuliza: Francis, Kwa Nini Nguvu Ya Motisha Huwa Haidumu?
Ipo Hivi
Motisha Ni Hisia.
Na Hisia Hubadilika Kila Siku.
↳ Kuna Siku Utajisikia Kufanya Kazi.
↳ Kuna Siku Hutojisikia Kabisa.
Kama Maisha Yako Yanategemea Motisha/Motivation…
Basi Kuwa Na Consistency Itakuwa Ngumu Sana.
Sasa...
Kama Wewe Ni Muhanga Wa Tabia Hii
Ngoja Nikupe Mbinu Ambayo Nimekuwa
Nikiitumia Kwa Muda Mrefu Sana Na
Kiukweli Imekuwa Ikinipe Matokeo Ya Uhakika
Upo Tayari?...
Kwanza Chukua Hii...
Watu Wanaopiga Hatua Kwenye Haya Maisha
Wana Kitu Tofauti.
Na Kitu Hicho Kinaitwa Mfumo. (System)
Mfumo Ambao Ndio Unawangoza Kufanya Chohote
Hata Pale Ambapo Hisia Zitayeyuka...
Chukua Hii ...
Badala Ya Kusubiri Motisha…
Jenga Mfumo Mdogo Wa Kila Siku.
Mfano:
• Muda Maalum Wa Kufanya Kazi
• Ratiba Rahisi Unayoweza Kuifuata
• Hatua Ndogo Unazofanya Kila Siku
Hata Kama Ni Kidogo…
Fanya Kila Siku.
Kwa Sababu Ukweli Ni Huu:
Motisha Inakufanya Uanze… Lakini Mfumo Unakufanya Uendelee.
Na Maisha Hubadilika Pale Unapokuwa Consistent…
Sio Pale Unapojisikia Kufanya Kazi.
Natumainio Leo Umepata Chochote Kitu Rafiki Yangu
Pia Kuna Tabia Nyingine Moja
Ambayo Inawafanya Watu Wengi
Wabaki Kwenye Mipango Tu Bila Kuchukua Hatua Halisi.
Tabia Ya Kufikiria Sana Kuliko Kufanya.
Tukutane Baadae...Maana Mambo Yameshakuwa Mengi Muda Mchache
Like Au Toa Reaction Yoyote
-🔥-👍-💪🏾 - 🙏🏽 - 🙌 - ❤️
Soon... Tukutane Kwenye Tabia Ya 9
...
FRANCIS | ABRACADABRA